MAELEZO YA TAMTHILIA
Msimu wa kwanza wa mfululizo wa tamthilia itwao “FROM” inaanza kwa kuonesha mji wa kutisha ulioko Marekani, ambao unawanasa watu wote wanaouingia. Usiku ukifika, viumbe vya kutisha hutokea kutoka msituni unaoUzunguka mji huo. Wakazi wa mji huo – wakiwemo watu binafsi na familia kutoka sehemu mbalimbali za Marekani – wanalazimika kukabiliana na changamoto za maisha yao mapya huku wakitafuta njia ya kutoroka kutoka kwenye mji huo wa ajabu.